Friday, February 15, 2013

China yazidi kuwekeza Afrika




Nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikinufaika na uwekezaji unaoendelea kufanywa na Serikali ya China na makampuni binafsi ya nchini humo katika sekta mbalimbali kwa lengo la kuukuza uchumi na kuondoa umaskini uliokithiri kwa wananchi.
Hatua hiyo inatokana na nchi hiyo kubwa duniani kuwa na uhusiano mzuri na Afrika katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijeshi, kijamii na kiutamaduni kuanzia  wakati wa Kiongozi wa kwanza wa Chama cha Kikomunisti cha China, Mao Zedong.
 Kuanzia karne ya  21  hali ya kisasa ya Jamhuri ya Watu wa China imezidi kujenga  nguvu ya uhusiano wa kiuchumi na Afrika.
Inaelezwa kuwa kuanzia Agosti 2007, inakadiriwa zaidi ya raia  750,000 China wanafanya kazi katika nchi za Afrika ambako kuna kuna makampuni ya nchi hiyo yamewekeza Afrika.
Raia hao wa China wengi wao wanafanya kazi katika makampuni ya ujenzi ukiwamo wa barabara, viwanda na sehemu nyingine.
Hali hiyo imezifanya nchi hizo za Afrika kunufaika kwa kukuza uchumi na baadhi ya raia wake kupata ajira.
Vilevile nchi hizo zimekuwa zikipata wataalaam wa fani mbalimbali kutokana na China kufadhili raia wao kwenda kujiunga na elimu ya juu katika vyuo vyake vikuu vilivyopo nchini humo.
 Hatua hiyo inawanufaisha wananchi wengi wa Afrika hasa wenye kipato cha chini kwa  kwa kununua bidhaa mbalimbali kwa matumizi ya nyumbani na nguo zinazozalishwa na makampuni ya China.
Vilevile vijana wengi wa wamejikuta wakijiajiri kwa kununua bidhaa hizo kwenye maduka na makampuni ya raia wa China na kuziuza huku wengine wakitembeleza mitaani na kujipatia kipato ambacho kinawawezesha kujikimu kimaisha.
 Hata hivyo, kitendo cha bidhaa za China kuuzwa kwa bei ya chini, kimekuwa kikilalamikiwa na wamiliki wa baadhi ya makampuni yanayotengeneza bidhaa kama hizo wakidai zinaua biashara zao na kuwa katika hatari ya kufilisika.
Makampuni hayo pia yamekuwa yakilalamikiwa kwa kuajiri raia kutoka China kufanya kazi hasa za vibarua ambazo zingeweza kufanywa na Watanzania.
 Biashara  hiyo kati ya China na Afrika iliongezeka zaidi katika miaka ya 1990 na kwa sasa  ni kubwa zaidi Afrika na kuzua hofu kwa baadhi ya mataifa mengine makubwa duniani kuwa bidhaa zake zinaweza kuua soko la bidhaa zao katika nchi mbalimbali kutokana na kuuzwa kwa bei ya chini na kuwa kimbilio na watu wengi hasa kwa Afrika.
  Mauzo ya bidhaa za China kwa nchi za Afrika yameteka soko kubwa katika baadhi ya nchi kutokana na kuuzwa kwa bei ya chini.
 Bidhaa hizo ni pamoja na vyombo vya jikoni, simu za mkononi, seti za redio, televisheni, miamvuli, nguo na vifaa vinavyotumia umeme.
China imekuwa ikichangia ukuaji wa uchumi wa Afrika kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali kwa nchi za Afrika.
Nchi hiyo imewekeza katika sekta hizo za biashara, madini, ujenzi wa miundombinu ya  barabara, reli, bandari, viwanja vya ndege na vya michezo .
Uwekezaji huo umeifanya biashara yake kuongezeka kwa kasi zaidi  zaidi ya miongo iliyopita.
Takwimu zinaonyesha kuwa kwa biashara ya jumla ilikuwa takribani dola bilioni 100  za Marekani mwaka 1990,   bilioni 500 mwaka 2000, bilioni 850 mwaka 2004, bilioni 1,400 mwaka 2005, na 2,200  mwaka 2007.
 Hata hivyo baadhi ya watu wamekuwa wakilalamikia bidhaa nyingi za nchi hizo kuwa hazina ubora wa viwango vinavyotakiwa.
Kwa upande wa Serikali ya China, imesema nchi za Afrika zinawajibika kwakushindwa kukamata  bidhaa zisizokuwa na ubora (feki) zinazoingizwa na wafanyabiashara  wenye tamaa.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara Mahusiano ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Lu Shaye, alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao walihudhuria mkutano wa tano wa Mawaziri katika Kongamano la Ushirikiano kati ya nchi za Afrika na China uliofanyika nchini humo.

Serikali hiyo pia imetangaza Tanzania ni moja ya eneo muhimu la biashara za bidhaa zinazozalishwa nchini mwake katika Afrika Mashariki kwa vileinazungukwa na  nchi za Ethiopia, Kenya,Msumbiji, Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Alisisitiza kuwa bidhaa za China ni bora na zinatambulika duniani na kwamba zinapatikana kwa  bei nzuri.

Habari zaidi zinasema kuna makubaliano ya  Chinakuwekeza katika nchi za Afrika kwa  kipindi cha miaka 10. 
Vilevile kuna habari zinaeleza kuwa maendeleo ya Afrika yanazivutia nchi zenye uwezo mkubwa wa kiuchumi duniani hasa China kwenda kuwekeza katika bara hilo .
pamoja na mambo mengine, China imeahidi kutoa mabilioni ya dola za Marekani kwa Afrika kuimarisha miundombinu,kufungua viwanda vipya na kuongeza ajira kwa vijana




No comments:

Post a Comment